Tanzania yaadhimisha siku ya hali ya hewa duniani

Naibu waziri wa Ujenzi,Uchumi na Mawasiliano  Injinia Edwin Ngonyani 

Muktasari:

  • Sherehe hizo hufanyika Machi 23 kila mwaka na kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Tuyaelewe mawingu na Umuhimu wake.’
  • Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Naibu waziri wa Ujenzi,Uchumi na Mawasiliano  Injinia Edwin Ngonyani  alisema katika kutambua  umuhimu wa kuongeza uelewa juu ya mawingu shirika hilo limeamua kutoa elimu kwa wananchi.

Dar es Salaam. Tanzania imeungana na wanachama 191 wa Shirika la Hali ya hewa Duniani (WMO) katika kuadhimisha siku ya hali ya hewa Duniani.

Sherehe hizo hufanyika Machi 23 kila mwaka na kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Tuyaelewe mawingu na Umuhimu wake.’

Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Naibu waziri wa Ujenzi,Uchumi na Mawasiliano  Injinia Edwin Ngonyani  alisema katika kutambua  umuhimu wa kuongeza uelewa juu ya mawingu shirika hilo limeamua kutoa elimu kwa wananchi.

"Usafiri wa anga na maji hutegemea sana utabiri wa hali ya hewa hasa wa saa na katika kuboresha hilo tumeamua kutoa elimu ya tabia ya mawingu kupitia makala mbalimbali katika televisheni,radio,magazeti,vipindi kwenye radio,mitandao ya kijamii", alisema 

Alisema Tanzania imekuwa nchi ya kwanza Afrika kushikiria tuzo ya utoaji taarifa za hali ya hewa zenye ubora kwa asilimia 80 hasa katika usafiri wa anga.