Tanzania yapewa masharti upatikanaji wa umeme

Muktasari:

Kauli hiyo imetolewa leo na Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa(UN OHRLLS) , Louise Stoddard wakati wa uzinduzi wa mkutano wa kimataifa kwa nchi Afrika kuhusu nishati endelevu.

Dar es Salaam. Tanzania itakuwa na wakati mgumu wa kuwezesha  wananchi wake kufikiwa na huduma ya umeme nchi nzima ifikapo 2030 endapo haitazingatia mambo matatu ikiwamo kuongeza vyanzo vya umeme , kuongeza kasi ya upatikanaji wa umeme na kudhibiti upatikanaji wa nishati hiyo.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa(UN OHRLLS) , Louise Stoddard wakati wa uzinduzi wa mkutano wa kimataifa kwa nchi Afrika kuhusu nishati endelevu.

Mambo hayo kwenye sekta ya Nishati ndiyo yatasaidia kufikia lengo namba saba katika Malengo Endelevu ya Millennium(SDG) ya 2030.

Tanzania imepewa heshima ya kuandaa mkutano huo wa siku mbili.

Ikiwa ni miaka 14 tu imebaki kufikia kilele hicho, Waziri wa Nishati Profesa Sospeter Muhongo alisema ni lazima kufikia malengo hayo kutokana na kasi ya usambazaji umeme inayoendelea.

"UN kuchagua sisi kuwa mwenyeji haikuwa bahati mbaya, wanaona kasi yetu.” alisema