Thibaut Courtois ajiandaa kutua Madrid

Thibaut Courtois 

Muktasari:

Taarifa kutoka ndani ya Chelsea zinasema kuwa Courtois aliyetwaa tuzo ya kipa bora wa fainali za Kombe la Dunia 2018 akiichezea Ubelgiji

London, England. Kipa wa Chelsea, Thibaut Courtois anajiandaa kuihama klabu hiyo na kwenda Real Madrid kwa ada ya uhamisho ya Pauni 35 milioni.

Taarifa kutoka ndani ya Chelsea zinasema kuwa Courtois aliyetwaa tuzo ya kipa bora wa fainali za Kombe la Dunia 2018 akiichezea Ubelgiji, ataondoka muda wowote kwenda Santiago Bernabeu.

Kipa huyo alikua akifuatiliwa na Madrid kwa kipindi kirefu na kufanya makosa mengi msimu uliopita kwa kipa Keylor Navas kunaonekana kumewasukuma Madrid kukamilisha uhamisho wake.

Courtois aliyekua akicheza kwa mkopo Atletico Madrid kati ya mwaka 2011 na 2014, familia yake ya mke na watoto wawili inaendeela kuishi jijini Madrid na inasemekana hilo lilifanyika makusudi kwa kuwa tangu wakati huo kulikua na mazungumzo ya kuhamia Real Madrid.

Kocha mpya wa Chelsea, Maurizio Sarri raia wa Italia, amekataa kufuata nyayo za watangulizi wake kumbembeleza kipa huyo abaki badala yake imebariki uhamisho wake na tayari ameanza kusaka kipa atakayeidakia klabu hiyo kwa furaha.