Tuesday, March 7, 2017

Tigo yajigamba mafanikio ya ‘Bima Mkononi’

Mkuu wa  huduma za kifedha kwa njia ya simu wa

Mkuu wa  huduma za kifedha kwa njia ya simu wa Tigo, Ruan Swanapoel 

By Ephrahim Bahemu, Mwananchi ebahemu@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Tigo imesema tangu ianze kutoa huduma ya bima ya matibabu, ajali na maisha kwa njia ya teknolojia ya simu, imepata wateja laki mbili.

Tigo walianza rasmi kutoa huduma hizo za bima Novemba mwaka jana.

Mkuu wa  huduma za kifedha kwa njia ya simu wa Tigo, Ruan Swanapoel amesema huduma hiyo ya bima ijulikanayo kama ‘Bima mkononi’ ni ya kipekee, rahisi na ya gharama nafuu.

Aliongeza kuwa huduma ya bima waliyoaianzisha  inaendana na maisha ya watanzania na ndicho chanzo cha kupokelewa vizuri na watanzania.

"Mpaka sasa tumeshalipa Sh 27 milioni kwa wateja wetu na gharama zetu za kujiunga ni rahisi ni kuanzia Sh 1,999 kwa mwezi kwa bima ya miezi miwili na 15,999 kwa bima ya mwaka mzima." amesema Swanapoel

-->