Tisa wakamatwa kwa kuandamana Dar

Muktasari:

Akizungumza na MCL Digital leo Aprili 26, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Lazaro Mambosasa amesema watuhumiwa hao wamekamatwa Mtaa wa Samora, Posta katikati ya mji.

 Jeshi la Polisi Kanda Maalumu limewakamata watu tisa kwa tuhuma za kufanya maandamano.

Akizungumza na MCL Digital leo Aprili 26, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Lazaro Mambosasa amesema watuhumiwa hao wamekamatwa Mtaa wa Samora, Posta katikati ya mji.

"Tumewakamata watuhumiwa tisa akiwamo, mwanafunzi wa Chuo cha Kilimanjaro kilichopo Mwenge akiwa na bango linalohamasisha maandamano," amesema Mambosasa na kuongeza:

“Tunaendelea kumhoji na wenzake wanane, tutakapokamilisha mahojiano hatua zaidi zitafuata.”

Kuhusu hali ya usalama Kamanda Mambosasa amesema jeshi limejipanga kuimarisha ulinzi usiku na mchana hakuna mtu yeyote atakayevunja sheria.