Thursday, June 14, 2018

Trump asherehekea siku ya kuzaliwa Singapore

 

Singapore. Maofisa wa Singapore wamemstukiza Rais wa Marekani  Donald Trump kwa kumfanyia sherehe ya siku yake ya kuzaliwa.

Maofisa hao walimstukiza kwa kumletea keki wakati wa chakula cha mchana nchini humo.

Rais huyo mwenye vituko ametimiza miaka 72 amefanyiwa sherehe hiyo huku akiwa hajui kinachoendelea ghafla alistuka tu anaimbiwa wimbo wa ‘happy birthday’ na maofisa hao.

 

“Sherehekea siku yako ya kuzaliwa ” aliweka kwenye mtandao wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Singapore Vivian Balakrishnan, muda mfupi baada ya tukio hilo akimpomgeza Trump

-->