Trump atishia kususia mazungumzo na Kim

Muktasari:

Katika mkutano wa pamoja na vyombo vya habari, yeye na Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe wamesema kuwa shinikizo dhidi ya Korea Kaskazini ni sharti liendelee kwa kukataa kusitisha utengezaji wa silaha za nyuklia.

Washington, Marekani. Rais wa Marekani, Donald Trump anasema kuwa iwapo mazungumzo yake na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un hayazai matunda 'atainuka na kuondoka katika mazungumzo hayo'.

Katika mkutano wa pamoja na vyombo vya habari, yeye na Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe wamesema kuwa shinikizo dhidi ya Korea Kaskazini ni sharti liendelee kwa kukataa kusitisha utengezaji wa silaha za nyuklia.

Abe yuko katika mgahawa wa Rais Trump wa Mar-a-Lago resort mjini Florida kwa mazungumzo.

Mapema, Trump alithibitisha kwamba mkurugenzi wa CIA, Mike Pompeo alifanya ziara ya kisiri hadi Korea Kaskazini ili kukutana na Kim Jong Un.