Tume ya Kudumu ya Uchunguzi yashughulikia malalamiko 71,000

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, Angela Kairuli

Muktasari:

Hayo yalisemwa leo (Ijumaa) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, Angela Kairuli alipokuwa akifungua Kongamano la  wadau kuadhimisha miaka 50 ya kuanzishwa kwa tume hiyo.

Dar es Salaam. Jumla ya malalamiko 71,000 yamepokelewa na kushughulikiwa na Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) katika kipindi cha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake.

Hayo yalisemwa leo (Ijumaa) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, Angela Kairuli alipokuwa akifungua Kongamano la  wadau kuadhimisha miaka 50 ya kuanzishwa kwa tume hiyo.

Waziri Kairuki amesema idadi hiyo ni ishara kuwa chombo hicho kina manufaa makubwa kwa wananchi wanyonge.

Amesema baadhi ya malalamiko yaliyopelekwa yalihusu vitendo vya unyanyasaji, masuala ya utumishi, malipo na mafao, mirathi, mgogoro ya ardhi na matumizi mabaya ya mali za Umma.