Tume yataka wazazi wawadadisi watoto wao

Muktasari:

Akizungumza leo (Ijumaa) Mkurugenzi wa THBUB, Francis Nzuki amesema wazazi kuwa karibu na watoto kunawawezesha kufahamu mambo mengi  wanayokumbana nayo.

Katika kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imewaomba wazazi kuhakikisha wanafuatilia maendeleo ya watoto wanaoishi nao na kuwachunguza iwapo wanafanyiwa unyanyasaji wowote.

Akizungumza leo (Ijumaa) Mkurugenzi wa THBUB, Francis Nzuki amesema wazazi kuwa karibu na watoto kunawawezesha kufahamu mambo mengi  wanayokumbana nayo.

“Hii ni zaidi ya kumuuliza kama amefanya ‘homework’ au amesoma nini darasani,” amesema.

Pia tume hiyo imeiomba Serikali kufanya marekebisho ya sheria kandamizi dhidi ya watoto na zile zinazokinzana na nyingine.

Nzuki amesema kuna jitihada kubwa zinazofanyika ili kuhakikisha sheria inayoruhusu mtoto kuolewa katika umri wa miaka 14 inabadilishwa kwani hii itasaidia kupunguza ndoa za utotoni.

 

“Tunaamini sheria hii itafanikiwa licha ya kukabiliana na mambo mbalimbali kama mila, tamaduni na dini mbalimbali lakini sisi tunaendelea kuhakikisha ndoa za utotoni zinapigwa vita,” amesema.