VIDEO: DC Kinondoni apokea mifuko 600 ya saruji

Muktasari:

Akipokea msaada huo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi alisema umekuja katika kipindi muafaka na utasaidia kuifanya shule hiyo kuwa ya kisasa.

Dar es Salaam. Kiwanda cha saruji cha Twiga kimetoa mifuko 600 ya saruji kwa ajili ujenzi wa madarasa nane, jengo la utawala na uzio katika Shule ya Msingi Ally Hapi iliyopo Bunju A.

Akipokea msaada huo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi alisema umekuja katika kipindi muafaka na utasaidia kuifanya shule hiyo kuwa ya kisasa.

"Tunataka Ally Hapi iwe mfano wa shule za kisasa katika Wilaya ya Kinondoni tunawashukuru wenzetu wa Twiga Cement kwa kutuunga mkono katika hili," alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Twiga Cement, Alfonso Velez alisema, "Tunafurahi kushiriki kwenye shughuli za kijamii na tuko tayari muda wote kuwa sehemu ya mafanikio yanayotokea ndani ya  jamii."