Ubakaji wampeleka jela maisha

Muktasari:

Akisoma hukumu hiyo juzi, Hakimu Sarafina Nsana alisema kutokana na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka haukuacha shaka, hivyo Mahakama imeridhia mshtakiwa kutumikia adhabu hiyo.

Nzega\Urambo. Mahakama ya Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, imemhukumu Salamba Makoye (24) kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na kosa la kumbaka mtoto mwenye miaka mitano.

Akisoma hukumu hiyo juzi, Hakimu Sarafina Nsana alisema kutokana na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka haukuacha shaka, hivyo Mahakama imeridhia mshtakiwa kutumikia adhabu hiyo.

“Kitendo alichokifanya kijana huyu mwenye akili timamu ilikuwa  makusudi, kwani muda wa kufanya kitendo hicho cha kikatili alipaswa awe kazini akizalisha na kuongeza kipato,” alisema Hakimu Nsana.