Uchaguzi mwingine wa Eala kufanyika Mei 10

Muktasari:

Kashilila ameliambia bunge leo kuwa uteuzi wa majina ya watakaogombea uchaguzi huo utafanywa na vyama Mei 3 na uchaguzi ni Mei 10.

Dodoma. Katibu wa Bunge, Thomas Kashililah, amesema uchaguzi wa wabunge wa bunge la Afrika Mashariki(Eala) utafanyika Mei 10 mwaka huu.

Kashilila ameliambia bunge leo kuwa uteuzi wa majina ya watakaogombea uchaguzi huo utafanywa na vyama Mei 3 na uchaguzi ni Mei 10.

Chadema ilishindwa kupata wawakilishi wa wabunge wa Eala baada ya majina waliyoyapeleka, kupigiwa kura ya hapana.

 Chadema kiliwateua Lawrence Masha  na Ezekia Wenje kuwania ujumbe wa bunge hilo la Eala.