Ugomvi wa kugombea laptop wasababisha askari kupoteza maisha

Muktasari:

  • Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema tukio hilo lilitokea Agosti 21 mwaka huu, Saa 10:00 usiku na na kumtaja aliyefanya mauaji hayo kuwa ni Magina Selemani (27) mkazi wa kigoto wilayani Ilemela ambaye alikuwa fundi wa computer.

Mwanza. Askari kwa kitengo cha upelelezi na makosa ya jinai Mkoa wa Mwanza, G.5092 Pc John Nyanga, ameuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu ya  shingoni katika eneo la villa pack club na mtu aliyekuwa na ugomvi naye.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema tukio hilo lilitokea Agosti 21 mwaka huu, Saa 10:00 usiku na na kumtaja aliyefanya mauaji hayo kuwa ni Magina Selemani (27) mkazi wa kigoto wilayani Ilemela ambaye alikuwa fundi wa computer.