Friday, April 21, 2017

Ujenzi wa mkongo wa taifa awamu ya tatu wakamilika

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa 

By Cledo Michael,Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.Tz

Dar es Salaam. Sekta ya Mawasiliano nchini imezidi kuimarika kutokana kukamilika kwa mradi Wa Ujenzi Wa Mkongo Wa Taifa awamu ya tatu ambapo watumiaji Wa Huduma za simu na intaneti wameongezeka nchini.

Hayo yamebainishwa leo (Ijumaa) na Katibu Mkuu Wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano anayesimamia Sekta ya Mawasiliano Dk.Maria Sasabo wakati Wa Kikao cha baraza la Wafanyakazi Wa sekta hiyo ili kujadili muelekeo Wa bajeti ya mwaka 2017/18.

Mhandisi Sasabo  alisema kuwa Matumizi ya laini za simu yameongezeka kutoka Milioni38.8 Desemba 2016 hadi kufikia 40 Milioni Desemba 2016.Pia,Idadi ya watumiaji Wa Intaneti imeongezeka kutoka watu 17 Milioni 2015 hadi 19.8 Milioni mwaka Jana.

"Kuwepo kwa Mkongo Wa Taifa wenye uwezo na ubora mkubwa unaoruhusu watoa Huduma wote kuutumia,umeleta faida nyingi ikiwamo kushuka kwa gharama na kuongeza upatikanaji wa huduma za Mawasiliano," alisema  Mhandisi Sasabo.

-->