Ujio wa Mfalme wa Morroco ni muhimu-Serikali

Mfalme wa Morocco, Mohamed VI .

Muktasari:

  • “Serikali ilishaeleza msimamo wake, kuna uhusiano wa aina nyingi, ujio huu ni muhimu kwa uhusiano wa kidemokrasia na uchumi kama hisia zitawatuma kufanya hivyo, wanapaswa kufuata sheria,” amesema Abass.

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania kupitia msemaji wake, Hassan Abass imesema ujio wa Mfalme wa Morocco, Mohamed VI ni muhimu kwa uhusiano wa kidiplomasia na uchumi.

“Serikali ilishaeleza msimamo wake, kuna uhusiano wa aina nyingi, ujio huu ni muhimu kwa uhusiano wa kidemokrasia na uchumi kama hisia zitawatuma kufanya hivyo, wanapaswa kufuata sheria,” amesema Abass.

Wakati mfalme  huyo akitarajiwa kuwasili leo nchini kwa ziara ya kikazi, huenda akapokewa kwa mabango baada ya vijana wanaounda kamati ya mshikamano wa Tanzania na Sahara Magharibi (TASSC) kujipanga kufanya hivyo kushinikiza nchi hiyo kuacha kuitawala kwa mabavu Sahara Magharibi.

Vijana hao wamefikia uamuzi huo kutokana na kile walichodai kusikitishwa kwao na kitendo cha Morocco kuendelea kuitawala kwa mabavu nchi ya Sahara Magharibi na kupuuza wito wa Umoja wa Mataifa (UN) unaoitaka kuipa uhuru nchi hiyo.