Saturday, November 18, 2017

Ukarabati MV Clarias, Umoja wakamilika

 

Mwanza. Zaidi ya Sh130 milioni zimetumika kukarabati meli za MV Clarias na Umoja zitakazofanya safari kati ya Ukerewe na Bukoba.

Akizungumza akiwa kwenye karakana ya ukarabati wa meli hizo, eneo la Mwanza South, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella alisema kwamba kukamilika kwa meli hizo kutapunguza adha ya usafiri kwa wakazi wa maeneo ya Bukoba, Ukerewe na kisiwa cha Kisumu.

Alisema kwamba meli hizo zinazofanyiwa ukarabati zina uwezo wa kubeba abiria na mizigo.

Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Mwanza, Erick Hamisi alisema meli hizo zinatarajiwa kuanza kazi baada ya miezi mitatu, wakati huo ukarabati mwingine wa meli za Butiama na Victoria unatarajiwa kukamilika baada ya miezi sita.

Alisema ukarabati wa meli hizo ni wa muda mfupi na kwamba kwa kipindi cha miaka miwili kutakuwa na meli nyingi zinazotoa usafiri kwa wakazi wa maeneo ya Kanda ya Ziwa. (Ngollo John)

-->