Ukawa, ACT wataka Magufuli afute siasa

Muktasari:

Kauli ya viongozi hao imekuja ikiwa zimebaki siku sita kabla ya Chadema kudai itafanya maandamano na mikutano ya hadhara nchi nzima katika operesheni waliyoiita Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta).

Dar es Salaam. Vyama vya upinzani vyenye uwakilishi bungeni vimesema iwapo Rais John Magufuli hapendi kukosolewa, apeleke bungeni muswada wa hati ya dharura wa kufuta vyama vyote vya siasa nchini.

Kauli ya viongozi hao imekuja ikiwa zimebaki siku sita kabla ya Chadema kudai itafanya maandamano na mikutano ya hadhara nchi nzima katika operesheni waliyoiita Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta).

Viongozi wa dini wamewakutanisha wanasiasa na Serikali ili kuiepusha nchi na shari kilichohudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba, James Mbatia (mwenyekiti, NCCR), John Mnyika (naibu katibu mkuu-Bara, Chadema), Mbarara Maharagande (mratibu mipango, CUF) na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

Juzi, Jeshi la Polisi liliongeza amri nyingine ya kupiga marufuku mikutano ya ndani ya kisiasa kwa madai ina lengo la kupanga uchochezi.

Viongozi kutoka vyama vya Chadema, NCCR-Mageuzi, ACT-Wazalendo na CUF jana walifanya mkutano wa pamoja na waandishi wa habari kuzungumzia kikao chao na viongozi wa dini kilichofanyika kwa siku mbili kuanzia Jumanne jijini Dar es Salaam na kueleza msimamo wao.

Akizungumza kwa niaba ya viongozi hao, Mbatia alisema hali halisi inavyoendelea nchini, inadhihirisha kuwa Rais Magufuli na Serikali yake hawataki uwapo wa vyama vya upinzani.

Habari zaidi soma Gazeti la Mwananchi