Ukawa: Kumpa notisi Sumaye ni kujenga Taifa la visasi

Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye.

Muktasari:

  • Juzi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alisema Sumaye amepewa siku 90 kuyaendeleza mashamba yake ya Mabwepande jijini Dar es Salaam na Mvomero mkoani Morogoro la sivyo atafutiwa hati ya umiliki wake.

Dar es Salaam. Siku chache baada ya Serikali kumpa notisi ya siku 90 Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye   ikimtaka kuyaendeleza mashamba yake kwa kipindi hicho, viongozi wa Ukawa wamesema kitendo hicho ni kutengeneza chuki endelevu na kujenga Taifa la visasi.

Juzi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alisema Sumaye amepewa siku 90 kuyaendeleza mashamba yake ya Mabwepande jijini Dar es Salaam na Mvomero mkoani Morogoro la sivyo atafutiwa hati ya umiliki wake.

Habari zinazohusiana

Hata hivyo, Sumaye ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chadema alisema notisi hiyo ni matokeo ya chuki za kisiasa baada ya kuihama CCM.