Ummy Mwalimu anena baada ya Mbowe kusema

Muktasari:

  • Ni kuhusu matibabu ya Lissu jijini Nairobi

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema kuwa ili Serikali kushiriki kwenye matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki(Chadema), Tundu Lissu ni lazima yawepo maombi.

Katika ukurasa wake wa Twitter, Ummy ameandika, “Mgonjwa alitolewa kwenye utaratibu wa Serikali alipopelekwa NRB. Sasa Gharama/Tiba zaid yahitajika. Serikali inaingiaje bila RidhaaYafamilia?

“Mgonjwa ni Mbunge, anahitaji matibabu zaidi. Lkn kwa kuwa sasa yupo nje ya utaratibu wa Serikali, Serikali kushiriki ni lazima yawepo maombi.”

Ummy ameandika hayo baada ya Yerico Nyerere kuhoji katika Twitter kuwa, “Wote tuliochangia matibabu na tunaoendelea kuchangia hatujaandikiwa barua na familia ya Lissu, ni @umwalimu tu ndie anasubiri barua rasmi.”