Wednesday, January 11, 2017

Upelelezi kesi ya ‘Mpemba’ wakamilika

 

By Tausi Ally, Mwananchi

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa upelelezi wa kesi ya kujihusisha na mtandao wa kihalifu na kukutwa na nyara za Serikali zenye thamani ya zaidi ya Sh 785 milioni inayomkabili Mpemba aliyetajwa na Rais John Magufuli, Yusuf Ali Yusuf na wenzake umekamilika na kesi imeahirishwa hadi Januari 24,2017.

Wakili wa Serikali, Patrick Mwita aliyaeleza hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa wakati kesi hiyo ilipotajwa.

Mwita alidai kuwa jalada la kesi hiyo lipo kwa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum Dar es Salaam (ZCO), Camilius Wambura ambaye analifanyia kazi, kisha atalipeleka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ambapo atalisoma na kulitolea maamuzi.

 

-->