Upepo wa siasa wabadilika nchini

Polisi wakipita kwenye mitaa mbalimbali ya mjini Singida jana kwa ajili ya kuwaonyesha wananchi silaha zilizonunuliwa kwa kodi zao. Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Singida, Mayalla Towo alisema zoezi hilo ni la kawaida na halina uhusiano na jambo lo lote. Picha na Gasper Andrew

Muktasari:

Mazungumzo ya wanasiasa, wachambuzi wa siasa na hata dola vinaonekana kujikita zaidi katika operesheni hiyo ya Chadema ambayo imepangwa kufanyika Septemba Mosi.

Dar\ Mikoani. Marufuku ya mikutano kwa viongozi wa kisiasa ambao hawakushinda kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka jana, operesheni Ukuta na mazoezi ya polisi katika mikoa yote vimebadili upepo wa kisiasa nchini.

Mazungumzo ya wanasiasa, wachambuzi wa siasa na hata dola vinaonekana kujikita zaidi katika operesheni hiyo ya Chadema ambayo imepangwa kufanyika Septemba Mosi.

Operesheni Ukuta, ambayo ilitangazwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe imezuiwa nchini kote huku Rais John Magufuli akikaririwa akisema kuwa hayupo tayari kujaribiwa.

Wakuu mbalimbali wa mikoa wametoa kauli za kuzuia operesheni hiyo kwenye maeneo yao, huku vikosi vya polisi vikionekana kufanya mazoezi katika miji mbalimbali nchini kujiandaa kukabiliana na operesheni hiyo, ambayo Chadema wamesema inalenga kupambana na kile walichokiita ukandamizwaji wa demokrasia.

 

Habari zaidi jipatie nakala yako ya Gazeti la Mwananchi