Urasmishaji wa majengo, upimaji viwanja kuongeza mapato ya Serikali
Muktasari:
Serikali imejipanga kuongeza mapato kwa kupanua wigo wa kodi
Dodoma. Serikali imesema itaendelea na urasmishaji wa majengo na upimaji wa viwanja ili kukuza mapato ya ndani.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alipokuwa anasoma bajeti ya Serikali kwa mwaka 2018/19 bungeni jijini hapa.
Akieleza kuhusu sera ya mapato kwa mwaka huo wa fedha, waziri alisema serikali imejipanga kuongeza mapato kwa kupanua wigo wa kodi na kuimarisha vyanzo vilivyopo.
Katika kutekeleza hilo, alisema mkakati uliopo ni: “Kurasmisha majengo na upimaji wa viwanja mchakato unaoendelea nchi nzima.’
Soma Zaidi: Dk Mpango: Rais alinitwisha msalaba wa zege