Ushindi wa Sitta Kinondoni wapingwa kortini

file photo

Muktasari:

Wadai katika shauri hilo ni Mustafa Muro na Jumanne Mbunju na wadaiwa ni Diwani wa Mikocheni  aliyechaguliwa kuwa Meya wa Kinondoni, Benjamin Sitta, Naibu Meya, Manyama Mangaru na msimamizi wa uchaguzi huo.

Dar es Salaam. Chadema kimefungua kesi Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kupinga uchaguzi wa meya na naibu wake kwenye Manispaa ya Kinondoni.

Wadai katika shauri hilo ni Mustafa Muro na Jumanne Mbunju na wadaiwa ni Diwani wa Mikocheni  aliyechaguliwa kuwa Meya wa Kinondoni, Benjamin Sitta, Naibu Meya, Manyama Mangaru na msimamizi wa uchaguzi huo.

 Mwanasheria wa Chadema, John Mallya alisema wanaiomba Mahakama kutengua matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika Jumapili iliyopita na iamuru uitishwe upya na wadaiwa walipe gharama za kesi hiyo.