VIDEO: Uwoya na Mobeto kikaangoni, watakiwa kuomba radhi

Uwoya

Muktasari:

TCRA yawataka kuomba radhi baada ya kuweka picha zao za utupu katika mitandao ya kijamii


Dar es Salaam. Kamati ya maudhui ya mamlaka ya mawasiliano  (TCRA) imewataka wasanii Hamisa Mobeto na Irene Uwoya kuomba radhi kwa kosa la kuweka picha za utupu mtandaoni.

Uamuzi huo uliochukuliwa baada ya wasanii hao kukiri kosa, umetangazwa leo Alhamisi Julai 19, 2018 mbele ya waandishi wa habari.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Vareli Msoka akiwa sambamba na wasanii hao amesema kutoka na kosa hilo wametakiwa kuomba radhi kupitia kurasa zao za kijamii na kuwa mabalozi kuhamasisha wenzao.

Kwa mujibu kamati hiyo,  Hamisa alifanya kosa la kuweka mtandaoni picha za ujauzito na Irene kuweka picha zake za nusu utupu, akiwa ufukweni.

Kufuatia kosa hilo,  Hamisa amepewa onyo na kutakiwa kuomba radhi kwa kuweka tangazo kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram.

Alipopewa nafasi ya kuzungumza,  Hamisa ameomba radhi na kuahidi kutorudia tena kufanya hivyo.

Kwa upande wake, Uwoya ameomba radhi na kuitaka kamati ya maudhui kutoa semina kwa wasanii ili kuwapa elimu kuhusu matumizi sahihi ya mitandao.