VIDEO: Lusinde: Wabunge CCM marufuku kukikosoa chama bungeni

Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde akichangia mjadala wa kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/2019, jijini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi

Muktasari:

Ametoa kauli hiyo leo bungeni mjini Dodoma

Dodoma. Livingstone Lusinde amewapiga marufuku wabunge wa CCM kukikosoa chama hicho tawala ndani ya Bunge.

Mbunge huyo wa Mtera (CCM) ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Juni 25, 2018 katika mjadala wa bajeti ya Serikali mwaka 2018/19, kusisitiza kuwa yeye ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho.

“Humu ndani tunapochangia tujiepushe na kazi za wengine. Eti tukifanya hivi tutashindwa sisi si wasemaji wa chama. Sisi wabunge wa CCM kazi yetu ni kuisimamia Serikali, kukosoa na kuitetea na nasema kama bosi wenu humu ndani ni marufuku kwa mbunge wa CCM kukizungumzia chama humu,” amesema.

“Hiki ni chama chenye Serikali na tupo hapa kuisimamia si kuikosoa CCM. Chama kushinda au kushindwa si sehemu yake hapa. Kama wabunge wangu hamna lugha ya kuisifia na kuikosoa tulieni.”

Kuhusu mvutano wa korosho amesema, “Humu ndani kuna wanasheria wengi, hivi wanashindwa nini kulitolea ufafanuzi hili la korosho likaisha. Sioni haja ya kutukanana katika hili.”