Vijana waliotekwa na wasiojulikana Pemba, wapatikana

Muktasari:

Waliopatikana ni Thuwein Nassor Hemed, Khamis Abadallah Mattar na Khalid Khamis Hassan.

Vijana watatu kati ya sita waliochukuliwa na watu wasiojulikana huko kisiwani Pemba, wamepatikana.

Vijana hao, wakazi wa Mtambwe, Kaskazini Pemba, Zanzibar, walichukuliwa majumbani mwao, Aprili 6 mwaka huu na watu waliokuwa na silaha.

 Waliopatikana ni Thuwein Nassor Hemed, Khamis Abadallah Mattar wameonekana katika eneo la Mzambarauni, Kaskazini Pemba, usiku wa kuamkia leo.

 Kijana mwingine, Khalid Khamis Hassan, amepatikana Likoni, eneo la Kojani, Pemba.

Akizungumza na MCL digital leo Aprili 15, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Haji Khamis Haji amesema ni kweli vijana hao wamepatikana usiku wa kuamkia leo huku hali zao za kiafya zikiwa haziridhishi.

Amesema kwa sasa vijana hao watatu, wanapata matibabu katika Hospitali ya Wete na baada ya kuimarika kwa afya zao watafanya mazungumzo nao ili kujua kwa undani juu ya tukio hilo.