Breaking News
Wednesday, December 13, 2017

Viongozi wa ACT Wazalendo Singida watimkia CCM

 

 Mwenyekiti na katibu wa Chama cha ACT Wazalendo mkoani Singida, wamejivua uanachana na vyeo vyao na kuhamia CCM.

Viongozi hao ni aliyekuwa mwenyeketi Wilfred Noel Kitundu na katibu wa mkoa wa chama hicho, Loth Robert Thomas.

Viongozi hao wamechukua uamuzi huo mbele ya mkutano mkuu wa uchaguzi CCM mkoa wa Singida uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Uhazili mjini hapa juzi.

Kwa nyakati tofauti walisema changamoto ambazo upinzani walikuwa wakizipigia kelele, Rais John Magufuli ameendelea kuzitatua kwa ufanisi.

Viongozi hao walikabidhi kadi za vyama vyao vya zamani, kwa mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Hadija Abood na kupewa kadi za CCM.

Katibu wa CCM mkoa wa Singida, Jimson Mhagama alisema kwamba wataendelea kuwapokea wanachama wanaorejea kutoka upinzani lakini ni lazima wafuate taratibu za chama.

(Gasper Andrew)

-->