Friday, July 21, 2017

Viongozi wa Chadema wakamatwa, wahojiwa na Polisi MbingaKatibu Mkuu wa Chadema, Vincent Mashinji

Katibu Mkuu wa Chadema, Vincent Mashinji 

By Mwandishi Wetu, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz

Songea.  Katibu Mkuu wa Chadema, Vincent Mashinji, mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe na wa Viti Maalumu, Zubeda  Sakuru wamekamatwa na Jeshi la Polisi wilayani Nyasa leo.

Taarifa iliyotumwa leo Jumamosi, Julai 15 kwa vyombo vya habari na Kitengo cha Mawasiliano cha Chadema, imeeleza kuwa viongozi hao wamepelekwa kituoni kuhojiwa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, viongozi hao walivamia kikao cha ndani cha Chadema kilichokuwa kikiendelea mjini hapo ikiwa ni sehemu ya ziara ya Dk Mashinji ya kukagua shughuli za chama katika kanda hiyo.

 

Tutaendelea kuwajuza kuhusu tukio hili

-->