Viongozi wa chama cha wakulima wa korosho wasimamishwa kwa ubadhirifu wa fedha

Muktasari:

Hatua hiyo imechukuliwa jana  baada ya mkaguzi wa Coasco kutoa taarifa ya mwaka 2015/2016 kwa wanachama  na kubaini matumizi mabaya ya fedha kiasi cha Sh 17milioni na kuibua mshtuko kwa wanachama wa ushirika.

Masasi.Viongozi wanane wa Bodi ya wakulima,   Nanyindwa wilayani Masasi,Mtwara (Coasco) wamesimamishwa uongozi kwa tuhuma za upotevu  wa fedha za wanachama wakulima wa korosha  Sh mil 17.

Hatua hiyo imechukuliwa jana  baada ya mkaguzi wa Coasco kutoa taarifa ya mwaka 2015/2016 kwa wanachama  na kubaini matumizi mabaya ya fedha kiasi cha Sh 17milioni na kuibua mshtuko kwa wanachama wa ushirika.

Kufuatia hali hiyo wanachama waliwakataa viongozi wa chama hicho na hivyo Mwakilishi wa mRajisi wa vyama vya ushirika nchini, Jeremiah Boniface alilazimika  kutoa tamko la kuisimamisha  kazi bodi ya chama hicho.