Virusi vya Homa ya Ini vyaupiku Ukimwi

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu

Muktasari:

Akizungumza na vyombo vya habari leo, Ijumaa Julai 28, Ummy amesema ugonjwa wa Homa ya Ini (Hepatitis B) unaongoza kwa kuua Tanzania baada ya maambukizi kufikia asilimia 16, huku Virusi Vya Ukimwi, ikiwa ni asilimia 5.3. 

Dar es Salaam. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema maambukizi ya ugonjwa wa Homa ya Ini yameongezeka mara mbili ya Virusi vya Ukimwi hivi nchini. 

Akizungumza na vyombo vya habari leo, Ijumaa Julai 28, Ummy amesema ugonjwa wa Homa ya Ini (Hepatitis B) unaongoza kwa kuua Tanzania baada ya maambukizi kufikia asilimia 16, huku Virusi Vya Ukimwi, ikiwa ni asilimia 5.3. 

Amesema ugonjwa huo huua taratibu ukilinganisha na magonjwa mengine kwa kuwa dalili zake huchukua muda mrefu kujulikana na kujitokeza wazi. 

Amesema licha ya kwamba mpaka sasa hakuna takwimu halisi kutokana na watu kutokuwa na tabia za kupima afya zao, idadi ya wagonjwa wanaobainika kuwa na homa hiyo wengi huwa  wamefikia hatua za mwisho za ugonjwa huo. 

"Tunapata takwimu hizi kupitia uchangiaji wa damu, damu inayokutwa na Homa ya Ini ni nyingi zaidi ikilinganishwa na ile yenye Virusi vya Ukimwi,"amesema Ummy.