Viziwi wapeleka kilio kwa Rais Magufuli

Rais John Magufuli

Muktasari:

Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Tanzania (Chavita) Taifa, Nidrosy Mlawa ametoa ombi hilo alipozungumzia kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Viziwi Duniani yanayofanyika kitaifa mkoani Tanga.

Tanga. Rais John Magufuli ameombwa kumteua mtaalamu wa lugha ya  alama atakayetafsiri hotuba na maelekezo yake kwenye mikutano na vyombo vya habari.

Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Tanzania (Chavita) Taifa, Nidrosy Mlawa ametoa ombi hilo alipozungumzia kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Viziwi Duniani yanayofanyika kitaifa mkoani Tanga.

Amesema walemavu wa kusikia wamekuwa hawapati kirahisi maelekezo ya Rais kutokana na kukosekana mtaalamu wa lugha ya alama kwa ajili yao.

Pia, amevilaumu vituo vya televisheni nchini kwa kushindwa kuweka wataalamu wa lugha hiyo hasa katika vipindi muhimu ikiwamo taarifa za habari.