Thursday, April 20, 2017

WB yashauri fursa za ajira kuongezwa

Mkurugenzi wa Benki ya Dunia (WB) kwa nchi za

Mkurugenzi wa Benki ya Dunia (WB) kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia, Bella Bird 

By Beatrice Moses, Mwananchi bmoses@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Benki ya Dunia (WB) kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia, Bella Bird amesema mkakati wa Tanzania katika kukuza uchumi, unaweza kusaidia kupunguza idadi ya watu wanaoishi kwenye mstari wa umaskini.

“Kufikia lengo hili kwa tathmini yetu inawezekan, ukichukulia rasilimali na uwezo wa Tanzania. Inahitaji kuangalia idadi ya watu ambao wanaishi chini ya mstari wa umaskini,” alisema Bird.

Miongoni mwa ahadi za Rais John Magufuli wakati akiwania wadhifa huo mwaka 2015 ilikuwa: “Nataka Watanzania wapate ajira, kazi ya Serikali itakuwa kukusanya kodi tu. Viwanda vinaweza kutengeneza ajira.”

Katika ripoti ya WD kuhusu Hali ya Uchumi wa Tanzania iitwayo ‘Fedha iliyo karibu,” iliyozinduliwa Aprili 11, imeibainisha kuwa Serikali inapaswa kutengeneza fursa za ajira kwa kujenga uwezo wa sekta binafsi, kuweka sera za kujenga mazingira salama kwa wawekezaji wa biashara kubwa au ndogo.

Hivi karibuni, kampuni mbalimbali nchini zimepunguza wafanyakazi kwa kile kinachoelezwa kuwa, ni kutokana na mdororo wa uchumi.

 

-->