Wabunge kupima Ukimwi

Muktasari:

kauli mbiu ya mjadala huo itakuwa ni ‘Ushiriki wa viongozi katika kufikia malengo ya 90 tatu.”

Dodoma. Mwenyekiti wa Bunge wa masuala ya Ukimwi, Rwegasira Oscar,  amesema wabunge wanatarajia kupima Ukimwi kwa hiyari Alhamisi Juni 21 shughuli itakayoenda sambamba na mjadala wa wazi juu ya ugonjwa huo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 19, 2018, jijini Dodoma, Oscar amesema mjadala huo utahudhuriwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na wabunge.

Oscar ambaye ni Mbunge wa Biharamulo Magharibi (CCM) amesema baada ya majadala huo unaoshirikisha taasisi zisizo za kiserikali na asasi za kiraia, zinazoratibiwa na Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na VVU  (Nacopha) kufanyika  Alhamis Juni 21, 2018, kutafanyika shughuli ya upimaji wa VVU/Ukimwi.

“Zitatolewa huduma za upimaji na matibabu ya VVU kwa waheshimiwa wabunge, ambao   watapima kwa hiyari,” amesema Oscar

Amesema kauli mbiu ya mjadala huo itakuwa ni ‘Ushiriki wa viongozi katika kufikia malengo ya 90 tatu.”