Wachakataji wa ngozi wakabiliwa na changamoto

Muktasari:

  • Kaimu Meneja wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (Sido) Mkoa wa Kilimanjaro, Arthur Ndedya alisema hayo jana wakati akizungumza na wadau wa uchakataji ngozi wilayani Mwanga.

Mwanga. Ukosefu wa mitaji, teknolojia na vitendea kazi ni changamoto kwa wachakataji wa ngozi hali inayosababisha washindwe kutengeneza bidhaa zenye ubora.

Kaimu Meneja wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (Sido) Mkoa wa Kilimanjaro, Arthur Ndedya alisema hayo jana wakati akizungumza na wadau wa uchakataji ngozi wilayani Mwanga.

Ndedya alisema wachakataji wa ngozi wamekuwa wakitumia zana za asili hivyo kushindwa kupata bidhaa zenye ubora.

Mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Mandela, Cecilia China alitoa ushauri kwa Serikali kupitia Wizara ya Mifugo kuwekeza zaidi kwenye teknolojia za kisasa ili wasindikaji wa ngozi wazalishe bidhaa zenye ubora.

“Ili tuweze kufaidika na idadi kubwa ya mifugo tuliyonayo, ipo haja ya kutoa elimu zaidi kwa wazalishaji wa bidhaa zitokanazo na ngozi.

Awali, akifungua warsha hiyo Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Aron Mbogho alisema vikundi ambavyo vinajishughulisha na usindikaji wa ngozi na utengenezaji wanahitaji kupatiwa elimu ili wafikie malengo wanayoyatarajia.