Wachimbaji wadogo waiangukia serikali -VIDEO

Wachimbaji Wadogo Waiangukia Serikali

Muktasari:

Akizungumza na waandishi jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa wachimbaji hao Thobias Rweyemamu amesema kuwa jumla ya makontena 60 yenye shaba na Nickel yamekwama katyika bandari ya Dar es Salaam kutokana na zuio la rais.

Dar es Salaam. Wachimbaji wadogo wa madini kutoka maeneo mbalimbali nchini wameiomba Serikali kuondoa zuio la kusafirisha kontena za madini jambo lililosababisha kupata hasara.

Akizungumza na waandishi jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa wachimbaji hao Thobias Rweyemamu amesema kuwa jumla ya makontena 60 yenye shaba na Nickel yamekwama katyika bandari ya Dar es Salaam kutokana na zuio la rais.

Alisema zuio hilo limewasababishia hasara kwani sasa hivi wanazidi kulipia makontena hayo gharama za kuyahifadhi kwenye maghala. Amesema kila siku wanalazimika kulipia dola 20 kwa kila kontena sawa na zaidi ya shilingi elfu arobaini.

Alisema mbali ya gharama hizo pia kuna ongezeko kubwa la gharama za kusimamisha migodi yao na kila siku hupoteza Sh milioni nne kwa ajili ya malipo ya wafanyakazi, mitambo, walinzi na matunzo ya vifaa.

Amesema ni takribani mwezi mmoja sasa tangu waache kjazi za uchimbaji kutokana na zuio la rais.