Wafuasi wataka Maalim aitishe mkutano kumtambua Lipumba

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad

Muktasari:

Baadhi ya wafuasi hapo wamekusanyika eneo la ofisi hiyo wakiwa na nia ya kumpokea Profesa Lipumba na kumzuia Maalim Seif endapo atafika.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake Juma Yassin amesema Maalim Seif ataendelea kubaki Zanzibar iwapo  hatataka kumtambua Profesa Lipumba ambaye ni mwenyekiti halali Kikatiba.
"Tumesikia leo huenda akaja lakini ofisi  na asijisumbue tupo tayari kwa lolote hadi amtambue Profesa Lipumba," amesema Yassin ambaye ni mwenyekiti wa Tawi la Kosovo Manzese.