Wafugaji Ikwiriri wakumbwa na mkono wa sheria

Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Bonaventure Mushongi alisema watuhumiwa wanashikiliwa katika Kituo cha Polisi Ikwiriri.

Muktasari:

  • Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Bonaventure Mushongi alisema jana watuhumiwa wanashikiliwa katika Kituo cha Polisi Ikwiriri baada ya msako uliofanywa kwa kushirikiana na raia.
  • Alisema polisi wanaendelea na msako ili kuwatia mbaroni watu wote waliohusika katika tukio hilo.

Rufiji. Wafugaji 14 wamejikuta matatani baada ya kudaiwa kuwajeruhi wakulima sita waliokuwa mashambani katika Kata ya Ikwiriri Mkoa wa Pwani.

Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Bonaventure Mushongi alisema jana watuhumiwa wanashikiliwa katika Kituo cha Polisi Ikwiriri baada ya msako uliofanywa kwa kushirikiana na raia.

Alisema polisi wanaendelea na msako ili kuwatia mbaroni watu wote waliohusika katika tukio hilo.

Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Ikwiriri, Iddi Malinda alisema wamewapokea majeruhi saba wakiwa na majeraha sehemu mbalimbali za miili yao.

Alisema miongoni mwa majeruhiwa hao, watatu wamepelekwa Hospitali ya Wilaya ya Rufiji.

Aliwataja majeruhi hao kuwa ni Adamu Jumanne, Mussa Adam, Abdalah Ibrahim, Fikiri Saidi, Matiko Masero, Mayasa Saidi na mmoja aliyetambulika kwa jina la Tingwa.