Wafungwa kufunzwa ufugaji nyuki

File Photo

Muktasari:

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mathew Mtigumwe amesema ufugaji bora wa nyuki utasaidia wananchi wakiwamo wafungwa kujikomboa kiuchumi.

Singida. Serikali mkoani hapa imejiwekea mkakati wa kuanza kutoa mafunzo ya ufugaji bora wa nyuki kwa wafungwa ili wakimaliza adhabu wakajiajiri uraiani.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mathew Mtigumwe amesema ufugaji bora wa nyuki utasaidia wananchi wakiwamo wafungwa kujikomboa kiuchumi.

“Takwimu zinaonyesha hadi kufikia mwisho wa mwaka jana, mkoa ulikuwa na mizinga ya asili 127,430 na ya kisasa 14,531. Mizinga hiyo inamilikiwa na watu binafsi na vikundi,” alisema.