Wageni, viongozi wamiminika JNIA kushuhudia uzinduzi wa ndege

Picha na Nuzulack Dausen, Mwananchi

Muktasari:

Licha ya mvua kubwa kuendelea kunyesha katika jiji la Dar es Salaam, lakini  wageni wanaendelea kuingia katika uwanja huo ili kushuhudia tukio hilo la kipekee.

Wakati Rais John Magufuli akitarajia kuzindua ndege mbili zilizonunuliwa kwa ajili ya Shirika la Ndege nchini (ATCL) leo, viongozi mbalimbali wakiongozwa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa wameanza kuwasili katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere.

Licha ya mvua kubwa kuendelea kunyesha katika jiji la Dar es Salaam, lakini  wageni wanaendelea kuingia katika uwanja huo ili kushuhudia tukio hilo la kipekee.

Jana ndege ya pili aina ya Bombadier Q 400 ilitua katika Uwanja huo ikitokea nchini Canada ilikotengenezwa.  Ndege ya kwanza iliwasili Septemba 20.