Wagoma watoto wao kuhamishwa

Wanafunzi wakiwa darasani

Muktasari:

Uhamisho huo unafanyika kutokana na maombi ya kamati ya shule hiyo kuomba igawanywe ziwe mbili kutokana na wingi wa wanafunzi.

Maswa. Wazazi wa wanafunzi 278 wa Shule ya Msingi Binza, wilayani hapa Mkoa wa Simiyu, wamegoma watoto wao kuhamishiwa Shule ya Msingi Shanwa kwa madai hawakushirikishwa.
Uhamisho huo unafanyika kutokana na maombi ya kamati ya shule hiyo kuomba igawanywe ziwe mbili kutokana na wingi wa wanafunzi.
Shule hiyo ina wanafunzi 1,100 hali inayodaiwa  kuwapa wakati mgumu walimu wa kutekeleza majukumu yao ya kufundisha kwa ufanisi.
Uamuzi huo ulifikiwa juzi katika kikao kilichowashirikisha wazazi, walimu wa shule za msingi Binza na Shanwa na maofisa elimu kutoka idara ya elimu wilayani hapa.