Tuesday, April 18, 2017

Wajasiriamali wakopeshwa Sh61 mil

 

By Mwanja Ibadi, Mwananchi mibadi@mwananchi.co.tz

Lindi. Halmashauri ya Wilaya ya Lindi, imevikopesha vikundi vya wanawake na vijana zaidi ya Sh61 milioni.

Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya hiyo, Rashid Namkulala alisema Sh43 milioni zimekopeshwa kwa vikundi 39 vya wanawake na Sh12 milioni kwa vijana.

Namkulala aliyasema hayo juzi wakati akitoa taarifa ya kufunga mafunzo ya wajasiarimali yaliyofanyika Kata ya Mtama.

Akikabidhi mikopo hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Mathew Makwinya aliwataka wajasiarimali kutumia mikopo hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa.

Makwinya aliwakumbusha wajasiriamali hao kurejesha mikopo hiyo kwa wakati ili zikopeshwa kwa wengine wenye uhitaji.

Aliwataka vijana kutumia fursa mbalimbali zilizopo wilayani humo badala kushinda vijiweni.

-->