Wajasiriamali wanaotumia teknolojia waombwa kuchangamkia fursa

Muktasari:

Shindano hilo ambalo ni la tano kufanyika nchini tayari washindi 8 waliopatikana wamewafikia na kuwasaidia jamii kwa zaidi ya vijana na watoto 10,000 kwa kutumia Tehama.
Mmoja ya washindi wa mwaka 2013, Faraja Nyalandu ambaye alianzisha programu ya Shule Direct inayosaidia wanafunzi kujifunza masomo mbalimbali kwa kutumia mtandao alisema elimu ndiyo msingi wa maendeleo ya nchi.

Dar es Salaam. Wajasiriamali wanaotumia teknolojia katika miradi yao nchini wametakiwa kuchangamkia fursa ya kujiandikisha katika shindano la Tigo Digital Changemakers ili kuweza kusaidiwa mitaji na mawazo ya miradi hiyo.

Shindano hilo ambalo ni la tano kufanyika nchini tayari washindi 8 waliopatikana wamewafikia na kuwasaidia jamii kwa zaidi ya vijana na watoto 10,000 kwa kutumia Tehama.
Mmoja ya washindi wa mwaka 2013, Faraja Nyalandu ambaye alianzisha programu ya Shule Direct inayosaidia wanafunzi kujifunza masomo mbalimbali kwa kutumia mtandao alisema elimu ndiyo msingi wa maendeleo ya nchi.

"Nchi haiwezi endelea bila elimu, na elimu inazingatia mambo matatu; mwalimu mzuri, kitabu na makundi kujadili hayo masomo na hivi vyote vipo katika hiyo programu mtandaoni," amesema Nyalandu.

Katika shidano hilo la mjasiriamali jamii mshindi atapata zawadi ya Sh40 milioni kwa ajili ya kuboresha mradi wake ili  uifikie jamii kwa kiwango kikubwa na uwe na manufaa.