Wajumbe wa kamati za makinikia wapongezwa Ikulu

Muktasari:

Taarifa iliyotumwa na Kurugenzi ya Habari na Mawasiliano ya Ikulu leo (Jumatano) imesema Rais amewapongeza wajumbe hao kwa kazi nzuri waliyoifanya.

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amekutana na wajumbe wa kamati zilizofanya uchunguzi wa mchanga wa madini katika makontena 277 yaliyozuiwa bandarini.

Taarifa iliyotumwa na Kurugenzi ya Habari na Mawasiliano ya Ikulu leo (Jumatano) imesema Rais amewapongeza wajumbe hao kwa kazi nzuri waliyoifanya.

Kamati hizo moja iliyoongozwa na Profesa Abdulkarim Mruma, ambaye timu yake ilichunguza kiasi cha madini kilicho kwenye mchanga huo na ya Profesa Nehemia Osoro iliyochunguza masuala ya kisheria kuhusu mchanga huo.

Rais Magufuli amesema timu hiyo imefanya kazi nzuri na yenye maslahi makubwa kwa Taifa na kwamba Serikali itahakikisha inafanyia kazi taarifa zilizotolewa na kamati hizo.