Serikali yaingia mkataba ujenzi wa barabara

Muktasari:

Profesa Mbarawa amesema kampuni zilizoomba zabuni zilikuwa 127.

Dar es Salaam. Serikali imesaini mkataba na wakandarasi wanne wa ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilomita 402 kwa thamani ya zaidi ya Sh702 bilioni.

Barabara hizo ni kuanzia Tabora, Usisula hadi Mpanda urefu wa kilomita 335 na Mbinga hadi Mbambabay urefu wa kilomita 67.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema fedha hizo ziliombwa kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).

Profesa Mbarawa amesema Desemba 4,2015 walipata fedha na kuanza mchakato wa kutafuta wakandarasi ulioanza Oktoba 2016. Amesema kampuni zilizoomba zabuni zilikuwa 127.

Amesema wakandarasi walioshinda ni kampuni za China Jiangxi Geo Engineeringi; Wu Yi; China Railways Seven Group; na China Henan International Corporation Group.