Wakulima wa umwagiliaji wavurugana

Mwanachama wa Skimu ya Umwagiliaji ya Mbuyuni iliyopo Kata ya Mapogoro wilayani Mbarali, Mkoa wa Mbeya,  Selemani Mwalwego  akizungumza kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa skimu hiyo uliofanyika jana. Picha na Godfrey Kahango

Muktasari:

Mtafaruku huo ulitokea kwenye mkutano mkuu wa kijiji hicho uliofanyika kijijini hapo juzi, wakulima hao walitaka kuwaondoa madarakani Katibu wa Skimu, Riziki Mwaisela, Mhasibu wao, Emmanuel Mseleka na wajumbe wa bodi.

Mbeya. Wakulima 150 wa mpunga ambao pia ni wanachama wa Skimu ya Umwagiliaji Kijiji cha Mbuyuni Wilaya ya Mbarali mkoani hapa, wamewatuhumu viongozi wa bodi ya kusimamia mradi huo kwa madai ya kufanya udanganyifu na matumizi mabaya ya madaraka.

Mtafaruku huo ulitokea kwenye mkutano mkuu wa kijiji hicho uliofanyika kijijini hapo juzi, wakulima hao walitaka kuwaondoa madarakani Katibu wa Skimu, Riziki Mwaisela, Mhasibu wao, Emmanuel Mseleka na wajumbe wa bodi.

Mkulima Azimio Mwangoje alisema viongozi hao hawafai kwa sababu wamepandisha ada ya shamba kutoka Sh15,000 hadi Sh50,000 bila kikao cha wakulima.

Hamza Gala alisema viongozi hao walighushi muhtasari na majina ya mahudhurio ya wanachama jambo ambalo linawakosesha imani na hawapo tayari kubariki kupanda kwa ada hiyo.

Gala alisema viongozi hao wameandika majina ya wananchi kuwa walihudhuria kikao ambacho hakikufanyika na kwamba, baya zaidi waliongeza gharama bila idhini ya wanachama.

Alishauri kutengua uamuzi huo, kitu ambacho kwa pamoja wanachama walikubali na kupanga kiwango kipya kutoka Sh15,000 hadi Sh10,000 kwa eka, ambayo mmiliki wa shamba atatakiwa kulipia kwa madai kuwa hivi sasa skimu hiyo ina miradi mingi ikiwamo mitambo ya kuvunia mpunga ambayo wanakodisha.

Mmoja wa viongozi hao, Scholar Mamboleo alikanusha tuhuma zote kwa niaba ya wenzake na kwamba, wapo tayari kujiuzulu kutokana na fitina iliyopo.

Mwenyekiti wa skimu hiyo, John Maharege alikiri viongozi wenzake kufanya tofauti na utaratibu na kuongeza ada ili kufidia deni la Sh46 milioni walizokopa kununua mtambo wa kuvunia.

mpunga.