Wednesday, January 11, 2017

Wamkalia kooni diwani kumiliki ardhi ya kijiji

 

By Baraka Rwesiga, Mwananchi brwesiga@mwananchi.co.tz

Chato. Diwani wa Kata ya Bwina mkoani Geita, Sospiter Nyamang’ondi ameingia matatani kuhusu eneo la ardhi, baada ya wananchi wa Kijiji cha Mulumba kudai anamiliki eneo lao kinyume na sheria.

Wananchi hao wanalalamikia eneo la eka sita wanalolitumia kupitishia mifugo yao, lakini Nyamang’odi anasema Nyamang’ondi anadai alilinunua kihalali zaidi ya miaka sita iliyopita.

Kutokana na hali wanamuomba Wakazi wa Kijiji cha Mulumba wamemwomba Mkuu wa Wilaya ya Chato mkoani Geita, Shaaban Ntarambe kuingilia kati mgogoro kati yao na diwani huyo.

Mkazi wa Kijiji hicho, Josiah Malima amedai eneo hilo limekuwa likitumika wakati wa kwenda na kurudi kutoka malishoni,  hivyo kitendo cha kumilikiwa ni kuwanyima haki.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kabusisi, Kihai Mabele ambaye eneo la mgogoro liko kwenye himaya yake amesema limekuwa likisababisha malumbano kwenye vikao vya wananchi huku pande mbili zinazohusika kila moja ikidai ni lake.

 Kaimu Ofisa Ardhi na Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Phinias Kagenda amesema kuwa ardhi ya vijiji hutawaliwa na sheria ya ardhi ya mwaka 2000 inayotoa mamlaka ya kupanga matumizi ya ardhi kwa Serikali ya vijiji kupitia mikutano mikuu ya wananchi.

 

-->