Wanafunzi 10 shule za msingi huacha masomo kila mwaka

Muktasari:

Akizungumza juzi kwenye kikao cha Baraza la Madiwani, Msafiri alisema utafiti uliofanyika kwenye shule mbalimbali wilayani humo umebaini kila muhula wanafunzi watano hukatisha masomo, jambo linaloathiri maendeleo ya elimu.

Kwimba. Mkuu wa Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza, Mtemi Msafiri amesema takwimu zinaonyesha kuwa wanafunzi 10 wa shule ya msingi hukatisha masomo kila mwaka wilayani humo kutokana na sababu mbalimbali.

Akizungumza juzi kwenye kikao cha Baraza la Madiwani, Msafiri alisema utafiti uliofanyika kwenye shule mbalimbali wilayani humo umebaini kila muhula wanafunzi watano hukatisha masomo, jambo linaloathiri maendeleo ya elimu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Maji wa wilaya hiyo, Peter Misalaba alisema wanafunzi 2,210 hawakufanya mtihani wa kuhitimu darasa la saba mwaka jana kutokana na utoro.

 Diwani wa Ngudu, Johansen Malifedha alishauri halmashauri kuandaa motisha kwa shule zinazofanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa na itolewe adhabu kwa walimu wakuu wa shule zinazoshika mkia.