Wanafunzi wabubujika machozi

Muktasari:

Wanafunzi hao walishindwa kijizuia baada ya kuwaona wenzao waliopata ajali huku wakikumbuka ajali hiyo.


Arusha. Wanafunzi wa darasa la saba waliobaki  katika shule ya Lucky Vincent wakiwa wanabubujikwa na machozi leo kukumbuka wenzao waliopoteza maisha kwenye ajali iliyotokea Mei mwaka huu na kuuawa watu 32.

Wanafunzi wa shule hiyo wakiimba wimbo wa kuwakaribisha wenzao walionusurika kwenye ajali hiyo ambao walienda Marekani.

Wanafunzi ambao walinusurika na kupelekewa kwa matibabu nchini Marekani waliorejea jana  ni Doreen mshana,Sadia Awadh na Wilson Tarimo