Wanafunzi wasoma chini ya mti

File Photo

Muktasari:

Kutokana na hali hiyo, wanafunzi hao hulazimika kupewa likizo msimu wa mvua ili kuepuka usumbufu wakati wa masomo.

Dar es Salaam. Wakati Serikali na wadau wa elimu wakiendelea kuchangia madawati nchini, wanafunzi wa awali katika Shule ya Msingi ya Kigezi, Manispaa ya Ilala wanasoma chini ya mti kwa kukosa madarasa.

Kutokana na hali hiyo, wanafunzi hao hulazimika kupewa likizo msimu wa mvua ili kuepuka usumbufu wakati wa masomo.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Kanuti Urasa amesema wana madarasa  tisa na yanayotumika ni saba, mawili yakiwa na nyufa.

Pia, amesema mabati yaliyoezekwa kwenye madarasa hayo yametoboka.