Wanahabari msilalamikie sheria- TEF

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Theophil Makunga amesema jana kuwa licha ya sheria kuwa na vifungu vyenye utata, haiwezi kuwa sababu ya kuwapa hofu wanahabari washindwe kufanya kazi zao.

Muktasari:

  • Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Theophil Makunga amesema jana kuwa licha ya sheria kuwa na vifungu vyenye utata, haiwezi kuwa sababu ya kuwapa hofu wanahabari washindwe kufanya kazi zao.

Dar es Salaam. Waandishi wa habari wametakiwa kufanya kazi kwa weledi na kuacha kulalamikia Sheria ya Huduma za Habari.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Theophil Makunga amesema jana kuwa licha ya sheria kuwa na vifungu vyenye utata, haiwezi kuwa sababu ya kuwapa hofu wanahabari washindwe kufanya kazi zao.

Akizungumza kwenye mkutano wa jukwaa hilo uliolenga kujadili namna ya kufanya kazi chini ya sheria hiyo iliofanyika hapa jana, Makunga amesema malalamiko hayatasaidia bali kinachotakiwa ni kufanya kazi kwa weledi zaidi.

Katibu wa Jukwaa la Wahariri Afrika Kusini, Reggy Moalusi amesema asilimia 80 ya waandishi wa habari nchini humo wana shahada ya kwanza.